» » Chadema kuwafungulia polisi kesi

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Kahama. Chadema kimesema leo kinatarajia kufungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Mwanza dhidi ya Polisi, kupinga zuio la maandamano mikutano ya hadhara ya kisiasa.

Akizungumza mjini Kahama jana, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alisema mikutano ya hadhara ni haki ya kikatiba na hawatanyamaza inapozuiwa na mtu, au mamlaka yoyote.

“Tutapambana kwa njia na nguvu zote kulinda demokrasia nchini, hata kama itabidi kufia uwanjani. Ikibidi kwenda mahakamani kudai haki hiyo tutafanya hivyo.” alisema

Hata hivyo, Mbowe hakuwa tayari kuthibitisha taarifa za Chadema kufungua kesi jijini Mwanza, leo.

Mawakili wa Chadema akiwamo Peter Kibatala na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu walitarajiwa kuwasili Mwanza jana tayari kutoa ushauri wa kisheria na kufungua kesi.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post