Sasa Jenerali Ulimwengu anaposema kuna viashiria vingi vya kuturudisha
nyuma miaka 50 kidemokrasia anazingatia tu historia ya nchi yetu
ilipotoka na ukweli kwamba historia hujirudia. Ni tahadhari muhimu
isiyopaswa kupuuzwa na mtu yeyote makini. Kumzodoa kwa maneno makali
makali hakuondoi UZITO wa hoja yake. Kama kuna hoja mbadala ziwekwe
mezani tuzisikie na kuzisoma.-Kitila Mkumbo
