Staa wa filamu za Kibongo, Hemed Suleiman ‘Hemed PHD’
Boniphace Ngumije, Risasi Jumamosi
MUUZA sura kwenye
filamu za Kibongo, Hemed Suleiman ‘Hemed PHD’ amefunguka kuwa japo ni
staa na mtu maarufu Tanzania lakini hata siku moja hajawahi kufikiri
kuwa atakuja kujihusisha kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa wa kike
kutoka Bongo kwa sababu anafahamu madhara yake.
Akipiga stori na Risasi Jumamosi,
PHD aliongeza kuwa madhara ya kutoka na staa kimapenzi husababisha
vyombo vya habari kuwamulika wahusika muda wote jambo ambalo yeye
halipendi ukizingatia anafuata misingi ya dini yake ya Kiislamu
inayomfanya aamini kuwa uhusiano ni suala binafsi ambalo halihitaji
kushereheswa na watu.
“Unajua vyombo vya habari vinapofahamu
kuwa unatoka na staa fulani vinaanza kukuandama wewe pamoja na huyo
mpenzi wako. Si kitu kizuri kwa sababu mnapotofautiana pia vinaanza
kuwazungumzia jambo ambalo wakati mwingine linaweza kusababisha hata
msirudiane kutokana na misteki tu ndogo. So mimi sipendi kabisa maisha
yangu yamulikwe ndiyo maana nimejiweka kando kwenye suala zima la
uhusiano kutoka na staa,” alisema PHD.
