» » Kanisa la Sinza Christian Center Latupiwa Vyombo Nje

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Kanisa la Sinza Christian Center limetupiwa nje vyombo vyake nje kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutokana na kanisa hilo kudaiwa deni la zaidi ya Sh. milioni 100. Aliyetekeleza agizo hilo leo ni dalali aliyepewa tenda hiyo Bw. Joshua ambaye aliteuliwa na Mahakama na jmiliki wa jengo hilo Bw. Prosper Rwendera.
Akizungumza wakati wa hamisha hamisha hiyo, mke wa mmiliki  wa jengo hilo, Bi. Patricia Prosper alisema; “Huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu.” 
Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.
 Magari yakiwa yanatolewa nje

 Kushoto kwa mbali ni Mke wa Miiliki wa Jengo hilo Bi. Patricia Prosper akiendelea na majukumu huku pembeni vijana wakipata maelekezo ya kuendelea kutoa vitu.

 Hili ni eneo la Kanisa hilo.


 Viti  vyote vikiwa vimetolewa nje.

  Vitu vikiwa nje ya Jengo hilo ambapo mpaka sasa kuna sinto fahamu vinapelekwa wapi.

 Vikombe nje.

 Vifaa vikiwa vimetolewa nje.
 Wametoa vitu vyote.
 Magodoro na vitanda vyote nje.
Baadhi ya Magari yaliyotolewa katika Jengo hilo ambapo hapo awali ilikuwa ni Kanisa

Source: Global Publisher
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post