» » Asilimia kubwa ya ukatili kwa watoto Arusha hufanywa na ndugu wa familia.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Watoto wengi wanaofanyiwa ukatili ukiwemo wa kubakwa na kulawitiwa  mkoani Arusha hawapati msaada wa kisheria kutokana na asilimia kubwa  ya vitendo hivyo kufanywa na watu wenye mahusiano na familia  husika  ambao licha ya kuficha ushahidi wanaamini kuwa kupeleka mashauri hayo  kwenye vyombo vya dola ni kujidhalilisha.

 Hali hiyo imesababisha watoto wengi kuendelea kufanyiwa ukatili   ambapo takwimu zilizotolewa katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa  Afrika zilizofanyika kata ya Themi zinaonyesha kuwa watoto wengi   wanaofanya vitendo hivyo ni wanafamilia na wamekuwa wanaficha    ushahidi.

Diwani wa kata ya Themi ambayo ni miongoni mwa zinazotajwa kukithiri  kwa ukatili wa watoto Bw Melance Kinabo na baadhi ya viongozi kuna  haja ya serikali kuangalia upya namna ya kushughulikia ukatili dhidi  ya watoto na jinsi ya kuwapata wanaendesha vitendo hivyo kwani muundo  wa sheria zilizopo sasa hivi unaonekana una mapungufu makubwa.

Naibu Meya wa jiji la Arusha Bi Viola Lazaro Meikoki amesema tatizo la watu kuficha ushahidi wa ukatili dhidi ya watoto ni kubwa zaidi  kwenye jamii zinazoendelea kudumisha mila na desturi ambazo zinaamini  kuwa masuala ya kifamilia yakishughulikiwa na vyombo vya dola  husababisha laana.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post