ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
Serengeti. Mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi
Mapinduzi, wilyani hapa, Mkoa wa Mara. Rehema Samson amegoma kunywa
dawa ya kinga inayotolewa bure kwa wanafunzi kwa ajili ya magonjwa
yaliyosahaulika (kichocho na minyoo) kwa madai hajawahi kutumia dawa za
hospitali toka azaliwe.
Baadhi ya wazazi inadaiwa wamewazua watoto wao wasipokee kinga hiyo
inayotolewa bure na Serikali kwamba ni ya Freemason. Imani hiyo
imekwamisha mpango huo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mapinduzi B’, Obwana Tom alikiri kuwa
siku ambayo dawa hizo zilitolewa, mahudhurio ya wanafunzi yalishuka.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO