Zaidi
ya watoto 50 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi kutoka
mikoa ya Kanda ya Ziwa, wamefanyiwa upasuaji katika hospitali ya Rufaa
Bugando na Madaktari bingwa sita kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI
).
Zoezi hilo la upasuaji kwa watoto 55 wenye matatizo ya vichwa
vikubwa na mgongo wazi kutoka mikoa ya Mara, Kagera, Mwanza, Kigoma,
Tabora, Shinyanga, Geita na Simiyu limeendeshwa na madaktari bingwa sita
wa upasuaji pamoja na wauguzi wanne kutoka Taasisi ya mifupa Muhimbili
na limeongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dk. Othman
Kiloloma.
Akina Mama wenye watoto walio na matatizo ya vichwa vikubwa na
mgongo wazi, ambao wamepata bahati ya kuonana na madaktari hao kwa ajili
ya matibabu ya bure ya watoto wao, wameushukuru uongozi wa hospitali ya
Rufaa Bugando kwa kukubali huduma hiyo kufanyika katika hospitali hiyo
na kuwaomba madaktari hao kulifanya zoezi hilo kuwa endelevu.