Wananchi
wanaoishi jirani na misitu na vyanzo vya maji mkoani Kilimanjaro
wamesema wanaweza kuyalinda maeneo hayo kwa gharama ndogo na ufanisi
mkubwa kuliko watendaji wa vyombo vya dola kama wakijengewa misingi
mizuri kwani wanazijua mbinu nyingi za wahalifu.
Wananchi hao wakiwemo walioshiriki kampeni za usafi katika Mlima
Kilimanjaro wamesema wakiwezeshwa wanaweza kuokoa nguvu na gharama
kubwa zinazotumika baada ya kutokea uhalifu na wangeweza
kuwadhibiti wahalifu kabla hawajasababisha hasara.
Msitu wa asili wa Mlima Kilimanjaro ni miongoni mwa inayokabiliwa
na changamoto ya uharibifu na uchafu iliyosababisha wadau wa uhifadhi
kuendesha kampeni ya siku kumi za usafi tatizo ambalo Mkuu wa Mkoa
wa Kilimanjaro Bw. Said Meck Sadik amesema lazima likomeshwe
Mlima huo wa Kilimanjaro licha ya kuwa kivutio kikubwa cha utalii
kinacholiingizia Taifa zaidi ya. Bilion 60 kila mwaka,pia kuna hazina
kubwa ya msitu wa asili wenye vyanzo vya maji vinavyotegemewa na idadi
kubwa ya wananchi wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini ,wanyama na viumbe hai
wengine