
Shirika
la ugavi wa umeme tanzania (TANESCO) mkoa wa Lindi,linakwama kufanya
shughuli zake kwa ufanisi kutokana na kuzidai taasisi za serikali pamoja
na watu binafsi zaidi ya shilingi Milioni Miasita.
Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya mkuu wa mkoa wa Lindi,
Godfrey Zambi, meneja wa TANESCO, mkoani Lindi,Johnson Mwigune, amesema
taasisi za serikali zinadaiwa zaidi ya shilinigi milioni mia tano, huku
watu binafsi wakiwa wanadaiwa zaidi ya shilingi milioni sabini.
Amesema deni hilo ni la mwisho wa mwezi huu, huku akisisitiza ili
shirika liweze kujiendesha na kufanya huduma za kimaendeleo ikiwa ni
pamoja na kusambaza umeme katika maeneo yenye maitaji linakwama
kutokana na fedha nyingi kuwa mikononi mwa taasisi za serikali.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ameomba taasisi
za serikali na watu binafsi, kulipa fedha hizo kwa wakati ili shirika
hilo liweze kujiendesha.
