» » Lowasa amewataka watanzania kutambua kuwa Chadema bado kipo imara na kinajengwa kitaalam zaidi.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Aliyekuwa mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya UKAWA kupitia Chadema na mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema Edward Lowasa amewataka watanzania kutambua kuwa Chadema bado kipo imara kitaendelea kuwatumikia na kwamba chama hicho hivi sasa kinajengwa kitalam zaidi.
Mh.Edward Lowasa ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na umati wa wapenzi wanachama mashabiki wa Chadema na watanzania wengine katika mjiji mdogo wa Mto wa Mbu wilaya ya Monduli ambapo pia amewataka watanzania kudumisha amani na kuwa na subira kwakuwa wakati wa utawala wa ukombozi wa Chadema  unakaribia.
SOURCE:ITV
 
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Salum Mwalimu amesema watanzania wanakila sababu ya kumshukuru Mh.Lowasa kwa utulivu aliyo uonesha baada ya uchaguzi na kuwa Lowasa anajali utu zaidi kuliko maslahi yake na mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Isack joseph akiahidi kutenda haki katika utawala wa Chadema kwenye Halshauri hiyo.
 
Katika mkutano huo pia watu wenye ulemavu walipata nafasi ya kutoa shukrani zao kwa wanasiasa baada ya uchaguzi mkuu wakidai panapo tokea machafuko wao ndiyo maathirika wakubwa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post