

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi |
PAZIA LIGI KUU YA VODACOM KUFUNGWA KESHO
Michezo
ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kufanyika
kesho Jumapili, Mei 22, 2016 kwa timu zote 16 kutinga katika viwanja
vinane tofauti kumaliza ngwe ya msimu wa 2015/16.
Michezo
itakayopigwa kesho ni pamoja na Simba itakayokipiga na JKT Ruvu kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Azam FC ambayo inawania nafasi ya
pili kama Simba, itakipiga na African Sports kwenye Uwanja wa Azam
Complex, ulioko Chamazi, Mbagala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa taarifa zaidi fuata link hapo chini
AIRTEL TANZANIA YAPANGA MIKAKATI YA MAENDELEO SOKA LA VIJANA
Kampuni
ya Airtel Tanzania jana Ijumaa Mei 20, 2016 imekutana na Shirikisho la
Mpira Tanzania (TFF) kuzungumzia mipango ya maendeleo wa mpira wa miguu
nchini ikiwa ni pamoja na michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel
Rising Stars inayotarajiwa kuanza Juni mwaka huu.
Katibu
Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine ambaye ndio aliongoza kikao hicho,
alitoa shukrani ka kampuni ya Airtel kwa kuwekeza kwenye soka la vijana
ambalo ndio msingi wa kukuza mpira wa miguu nchini. “Naamini ya kwamba
kwa kuendelea kuwekeza kwenye soka la vijana, tutaweza kufika mbali kwa
kupata matokeo mazuri.”
Kwa taarifa zaidi fuata link hapo chini
