ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
Mpatanishi wa mgogoro wa Burundi, Benjamin Mkapa
Arusha, Tanzania. Mpatanishi wa mgogoro wa Burundi, Benjamin Mkapa
ameahidi kuzungumza na pande zote hasimu nchini Burundi katika jitihada
za kuutatua mgogoro wa nchi hiyo ndogo ya katikati mwa Afrika. Mkapa
ambaye alikuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu wa Tanzania jana alitoa
taarifa na kusema kuwa atazungumza na makundi yote hata watu ambao
hawashiriki katika mazungumzo ya Arusha ya kujadili mgogoro huo. Alisema
ni wazi kuwa kama upande wa upinzani utashiriki, utazidi kuyapa maana
mazungumzo hayo.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO