» » Atupwa jela kwa kutunga shairi kwenye uume wake Myanmar

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Maung Saungkha (katikati) akiwa chini ya ulinzi baada ya kufikishwa mahakamani mjini Rangoon jana kujibu mashtaka ya kukashifu jina la rais na kutiwa hatiani. Picha ya Mtandao 
Rangoon, Myanmar. Hakika duniani kuna mambo na ukishangaa ya kusini basi subiri kuduwazwa na yale ya kaskazini.

Mkazi mmoja nchini Mynmar amejikuta akitupwa jela kutumikia kifungu cha miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya kutunga shairi na kisha kuchora sura ya rais katika sehemu zake za siri.

Waendesha mashtaka walieleza mahakamani kuwa mtu huyo ambaye ametambulika kama mwandishi, alitunga shairi kwa kuchora sura ya Rais wa Mynmar, Thein Sein kwenye uume wake.

Maung Saungkha amehukumiwa kwa kosa la kumharibia mtu sifa mtandaoni baada ya kuchapisha shairi hilo katika mtandao wake wa kijamii wa Facebook.

Saungkha mwenye umri wa miaka 24 ambaye kwa sasa anafahamika zaidi kwa jina la ‘penis poet’ ameanza kutumikia kifungo hicho na wakili wake hakueleza chochote kama atakata rufaa kupinga hukumu ya mteja wake huyo.

Awali, mtuhumiwa huyo akikuwa mafichoni akikwepa mtego wa polisi waliokuwa wakimsaka kwa muda mrefu baada ya picha za shairi hilo kuanza kuzagaa mitandaoni. Ingawa alifanya kosa hilo kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopita, waendesha mashtaka walidai Saugkh alikuwa amemdhihaki kiongozi wa taifa hilo.

Katika utetezi wake Saungkha alidai kuwa hakuna sehemu katika shairi hilo ametaja jina la rais, utetezi huo ulipuuzwa na mahakama baada ya kupokea hoja ya waendesha mashtaka.

Mamlaka kuu nchini Mynmar inaendelea kuwafunga raia wake jela kwa kutoa maoni kwenye mitandao ya kijamii ambayo yanaikosoa Serikali.

Baadhi ya watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakishutumu hatua ya kubana uhuru wa maoni, lakini wale wanaopendelea zaidi uhuru wa faragha wamelaumu kitendo cha mwandishi huyo kutunga shairi hilo.

Hivi karibuni Serikali mpya ya Myanmar ya Aung San Suu Kyi inayongozwa na Rais Htin Kyaw iligonga katika vichwa vya habari baada ya kuamuru kuachiwa kwa kundi la pili kubwa la wafungwa wa kisiasa nchini humo.

Kundi la wafungwa wapatao 100 liliachiwa huru mapema mwezi huu na baadaye kufuatiwa na lingine. Maofisa walisema hatua hiyo ya kuwaachia wafungwa wa kisiasa ambayo ni miongoni mwa maamuzi makuu ya kwanza yaliyoanza kutekelezwa na Serikali ya San Suu Kyi’s, itaendelea.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post