wakizungumza na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo kwa
ajili ya kufuatilia tukio hilo,mwenyekiti wa kijiji hicho,Samwel Fransic
pamoja na mkunga wa kijiji hicho,Christina John wanaelezea tukio hilo.
Akizungumza tuhuma za mganga huyo Mkurugenzi wa Halmashauri wa
wilaya hiyo,Naomi Nko amesema tayari ofisi yake imeshapokea malalamiko
ya mganga huyo na tayari ameshamchukulia hatua ya awali ya kumsimamisha
kazi wakati akisubiri taratibu nyingine za kisheria .
Akiongea kwa njia ya simu kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa
Polisi mkoa wa Mara ,Ramadhani Ngh’azi amesema jeshi hilo linamshikilia
mganga huyo kwa uchunguzi zaidi ili kubaini kama kweli alizembea na
kusababisha kifo cha mtoto huyo na endapo itabainika atafikishwa
mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamewaeleza waandishi
wa habari kuwa mganga huyo alikuwa ameshakataliwa kijijini hapo na
tayari walikuwa wameshakaa mkutano wa kumkataa kutokana na vitendo vyake
vya kutozingatia maadili ya kazi yake.