» »Unlabelled » Wadaiwa wajinyonga kutokana na msongo wa mawazo

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Tabora. Wanawake wawili wamefariki dunia kwa kujinyonga katika matukio mawili yaliyotokea mikoa ya Geita na Tabora yanayohusishwa na msongo wa mawazo.

Wakazi hao ni  Mwajuma Hamad, Mkazi wa Miyogoni, Manispaa ya Tabora, ambaye alijinyonga chumbani kwa kile kinachodaiwa ni kuchukizwa na kitendo cha mume wake, Juma Kiligito kumzuia kujihusisha na ujasiriamali wa ushonaji nguo, huku mwenzake Anastazia Kahezi (65), mkazi wa Kijiji cha Nyarututu Wilaya ya Chato mkoani Geita alijinyonga kwa kusongwa na mawazo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi, huku Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akiwaomba wenye taarifa kujitokeza kusaidia upelelezi
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post