» »Unlabelled » Picha: Mrirthi wa Kanumba Aunguzwa na Kemikali Usoni

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

kanumbaaa222

Fredy Swai (kushoto) na Kanumba enzi za uhai wake.
Kumekuwa na tatizo kubwa katika mfumo mzima wa uandaaji wa filamu hapa Tanzania hasa katika suala la kuandaa wasanii ili kuleta uhalisia wa kazi husika.

…Baada ya kuumizwa.
Kiajana aliyetambuishwa na mama wa aliyekuwa nguli wa filamu hapa nchini, Steven Kanumba, Flora Mtegoa kuwa ndiye mrithi wa mwanane huyo kwenye tasnia ya uigizaji, Fred Swai amekumbwa na balaa ambalo ameeleza kuwa hatolisahau katika maisha yake baada kuunguzwa vibaya na kemikali usoni katika harakati za kuandaa filamu.
Akizungumza kwenye Kipindi maalum cha Exclusive Interview kupitia Global TV Online, Swai amesema kuwa siku hiyo aliitwa kwenda kucheza kipande cha muvi ambacho alitakiwa aigize kama mgonjwa.
Jeraha la Fredy.
Hivyo muandaaji alimtaja afungwe bandeji usoni ili kuonesha uhalisia wa mgonjwa, ambapo bandeji hiyo ililowanishwa na kemikali zinazotumika kusafishia vidonda, iodine solution.
Swai aliendelea kueleza kuwa, badala ya kulowanishiwa iodine ya kawaida isiyo kali (diluted solution) aliwekewa concentrated iodine ambayo ni kali zaidi hivyo kuunguza sehemu ya paji la uso.
Hii imekuja ikiwa ni siku chache tu baada ya Muigizaji wa Nigeria, Kuchomwa Moto wakati wakishuti video.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post