Inadaiwa kuwa mtuhumiwa akiwa amelewa alifika maeneo ya nyumbani anapoishi mtoto huyo kisha akamtuma dukani maeneo ya mwaloni Igombe.
Aidha baada ya muda mchache kupita mtuhumiwa alimfuata mtoto huko dukani kisha kumfanyia ukatili wa kumbaka na kusababisha majeraha na maumivu makali katika sehemu za siri za mtoto huyo.
Wananchi walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo, askari walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye yupo katika mahojiano na jeshi la polisi, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Msangi amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha tukio hili ni ulevi. Mtoto amepatiwa matibabu hospitali na hali yake inaendelea vizuri.