Tuesday, December 13, 2016

Waziri wa zamani wa Serikali ya Awamu ya Tatu, William Kusila (72) amemshauri mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kukifumua chama hicho ili akisuke upya kwa lengo la kukirudisha kwenye misingi yake.
Kusila alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika kijijini kwake Mtitaa, Kata ya Mtitaa wilayani Bahi, takriban kilomita 57 kutoka mjini Dodoma.
Kusila alisema hayo wakati CCM ikielekea kufanya mkutano wa Halmashauri Kuu, ambayo ni chombo cha pili cha juu cha uamuzi baada ya Mkutano Mkuu.
“CCM kilishakuwa kichafu, kilikuwa kichaka cha wala rushwa, wezi, majambazi, wauza dawa ilimradi tu mtu yeyote aliyekuwa na matatizo yake, kimbilio lake lilikuwa ni CCM,” alisema.