» »Unlabelled » Picha: Daladala lilivyoacha njia na kupinduka leo Mbagala, DSM

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Monday, December 12, 2016


Wananchi wakiangalia daladala lenye namba za usajili T 161 CRP lililoacha njia na kupinduka Mbagala Misheni kwa Bluda Dar es Salaam leo asubuhi na kujeruhi watu watatu.

                                                              Daladala likiwa mtaroni.


WATU watatu wamejeruhiwa vibaya baada ya daladala walikuwa wamepanda kutoka Temeke kwenda Mbagala Kuu kuacha njia na kupinduka jijini Dar es Salaam.

Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi wa Temeke ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa polisi alisema ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 na nusu asubuhi. 

Alisema daladala hilo liliacha njia na kutumbukia kwenye mtaro eneo la Mbagala Misheni kwa Bluda baada ya kuteleza kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha.

Alisema baada ya ajali hiyo wananchi walifika kutoa msaada kwa majeruhi ambao walikimbizwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu.

Alitaja daladala hilo kuwa ni lenye namba za usajili T 161 CRP ambapo alitoa mwito kwa madereva kuwa waangalifu wanapoendesha magari yao hasa katika kipindi ambacho mvua zinanyesha.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post