» »Unlabelled » Babu wa miaka 81 atafuta klabu mpya ya kuchezea Uingereza

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 Tuesday, December 13, 2016

Mchezaji kandanda wa umri wa miaka 81, anayeaminika kuwa mchezaji soka mkongwe zaidi nchini Uingereza, anatafuta klabu mpya.

Dickie Borthwick
Dickie Borthwick alianza kucheza soka mwaka 1947 akiwa na miaka 12

Dickie Borthwick, anayetoka Weymouth, Dorset, alianza kucheza kandanda mwaka 1947 akiwa na miaka 12.

Alikuwa mchezaji katika klabu ya wanajeshi wastaafu ya Wyke kabla ya klabu hiyo kuvunjwa. Hata hivyo, anakiri kwamba huenda umri umemzidi na haitamfaa kucheza kwenye ligi ya wanajeshi wastaafu tena.

ALiambia gazeti la The Mirror nchini Uingereza kwamba amepokea mwaliko wa kujiunga na klabu ya soka ya matembezi lakini amesema anataka kushiriki soka yenye kasi kiasi.

Dickie Borthwick
Mr Borthwick anasema amefunga zaidi ya magoli 400 katika miaka 69 aliyocheza kandanda

Mr Borthwick anasema amefunga zaidi ya magoli 400 katika miaka 69 aliyocheza kandanda

Bw Borthwick, ambaye alitibiwa saratani ya tezi dume miaka mitatu iliyopita, anasema bado yuko sawa kiakili na kimwili na bado anaweza kukimbia na kusakata gozi.

Anasema anatumai wachezaji wa klabu ya soka yakutembea, ambayo imempa mwaliko, wanaweza kufanya mazoezi na labda waongeze kasi kwenye mchezo wao.

Amesema yuko tayari kujiunga na klabu yoyote ya wazee wa zaidi ya miaka 60 eneo la Dorset.
Anasema amefunga mabao 400 katika miaka 69 aliyocheza soka na hajawahi kuadhibiwa mchezoni katika mechi zote rasmi 1,600 ambazo amewahi kucheza.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post