Monday, December 12, 2016
Antonio Guterres kutoka Ureno ameapishwa leo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mbele ya wawakilishi wa nchi 193 wanachama wa Umoja huo.
Ndani ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Baraza Kuu, Peter Thomson akiitisha kikao mahsusi kwa ajili ya kuapa kwa katibu Mkuu wa Tisa, Antonio Guterres.
Mwakilishi wa kundi la Asia na Pasifiki, akawasilisha azimio namba… mahsusi la kuchaguliwa rasmi kwa Guterres …ambapo Bwana Thomson akauliza wajumbe wa Baraza iwapo wanaridhia au la..
Hatua hii ilifuatiwa na matamko kutoka kanda mbali mbali zinazowakilishwa kwenye Umoja wa Mataifa na hatimaye kiapo..
Guterres ingawa ameapa leo, ataanza rasmi majukumu yake tarehe Mosi Januari mwakani baada ya Katibu Mkuu wa sasa Ban Ki-moon kuhitimisha jukumu lake la miaka kumi tarehe 31 mwezi huu.