» »Unlabelled » Anne Makinda ametoa siku saba kwa msimamizi wa Jengo la NHIF kukamilisha hili

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Tuesday, December 13, 2016

SPIKA Mstaafu wa Bunge la Jumuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Anne Makinda, ametoa siku saba kwa msimamizi wa Jengo la Mfuko huo linalojengwa Jijini Mbeya, kutoa maelezo ya kina , kwa nini jengo hilo halijamalizika kwa wakati na lini litakuwa limemalizika.

Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya NHIF Anne Makinda anasema kwa mujibu wa mkataba, jengo hilo lilipaswa kumalizika julai mwaka jana lakini hadi sasa bado, akisema NHIF ilijenga kama mradi hivyo kuchelewa kukamilika kunaweza kuwafukuza wateja walionesha nia ya kukodi.

Awali Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF ametembelea na kugua ujenzi wa wadi ya watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya,na kukabidhi mifuko 100 ya saruji kwa niaba ya waziri wa Afya Ummy mwalimu ambaye aliahidi, akapongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa ujenzi akisema utaondoa adha kwa wagonjwa hususani watoto kwa kuwa hata maambukizi ya magonjwa ya watu wazima hayatakuwepo, lakini akapongeza hospitali hiyo kutumia mikopo ya NHIFkwaajili ya vifaa tiba.

Baadae Mwenyekiti wa Bodi akatembelea kitengo cha wazazi meta na kujionea hali ilivyo.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post