Wakizungumza na Camera ya Channel Ten iliyofika kituoni hapo kwa ajili ya kujionea hali halisi ya ya Usafiri kwa mabasi yaendayo mikoani abiria hao wamesema kuwa kama ilivyo kwa misimu mingine ya sikukuu kwa miaka iliyopita msimu huu pia hali ya usafiri ni ngumu kutokana na mabasi mengi kusheheni abiria huku abiria wengine wakishindwa kupata nafasi za kusafiri kutokana na ongezeko kubwa la abiria ambapo pia nauli zanadaiwa kupanda kwa baadhi ya mabasi huku mabasi mengine nauli zikibaki kama zilivyokuwa hapo awali…
Licha ya changamoto ya uchache wa Mabasi yaendayo mikoani pia Abiria hao wamelalamiikia uongozi wa kituo hicho kwa kutoweka sehemu za kupumzikia abiria wakati wa kusubiria usafiri wa mabasi licha ya kutozwa ushuru wakati wa kuingia kituoni hapo.