Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani DCP Mohamed Mpinga akizungumza wakati wa Ufungaji mafunzo ya waendesha bodaboda 1200 yaliyokuwa yakitolewa na chuo cha ufundi Polisi – Kurasini amesema kutokana na mafunzo hayo wanatarajia kuwa na mabadiliko makubwa ya utii wa sheria za usalama barabarani lakini pia kutojihusisha na Uhalifu kwa wahitimu hao.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda, Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amewataka waendesha bodaboda kushirikiana na jeshi la polisi katika kupiga vita uhalifu wa kutumia silaha ,kwa kuwabaini wahusika lakini pia akiwashauri kujiunga na mifuko jamii hasa katika kipindi ambacho mwonekano mpya utaanza kuonekana kuanzia mwezi januari baada ya kuweka utaratibu maalum wa kutambulika kila bodaboda katika jiji la dsm.