ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
DAR ES SALAAM: Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amepiga
marufuku kampuni zinazohusika na suala la kukusanya ushuru wa maegesho
ya magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kuacha kufunga minyororo
kwenye magari ambayo yanaengeshwa ndani ya muda mfupi, na kuagiza kuwa
wanapaswa kusubiri mpaka saa moja ipite, endapo mwenye gari atakuwa
hajatokea ndiyo waendelee na taratibu nyingine.
Pia Meya Mwita amewataka wafanyakazi wa kampuni hizo, kuhakikisha muda
wote wanavaa sare ili iwe rahisi kuwatambua.Ameongeza kuwa hadi sasa,
tayari zimepatikana zaidi ya mashine 850 ambazo kuanzia Januari, 2017
zitaanza kutumika kukusanyia ushuru wa maegesho ya magari, tofauti na
sasa ambapo risiti za kawaida zinatumika.
Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wanadhibiti mapato
yanayopatikana kutokana na maegesho ya magari, ili fedha hizo ziweze
kutumika kwa shughuli nyingine na kuboresha miundombinu.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO