» »Unlabelled » Wananchi Morogoro, Wagomea michango ya maendeleo

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Miradi ya maendeleo katika kijiji cha njungwa,kata ya Mandege wilayani Gairo mkoani Morogoro imekwama kukamilika,huku wananchi wakigomea kuchangia michango ya maendeleo kutokana na kushindwa kusomewa taarifa za mapato na matumizi tangu mwaka 2014 na kulalamikia matumizi mabaya ya fedha.
wananchi wa eneo hilo wamelalamikia ushirikiano mdogo baina ya viongozi wa kijiji na kata jambo lililofanya kushindwa kufahamika matumizi ya fedha za maendeleo,ikiwemo zaidi ya shilingi milioni sita walizodai haziendani na miradi ya maendeleo iliyopaswa kufanyiwa matengenezo ikiwemo zahanati na choo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo Agness Martin aliyeanza kazi Julai mwaka huu ameeleza kutodhirishwa na taarifa iliyotolewa na viongozi wa eneo hilo na kubainisha  taarifa za mapato na matumizi zinapaswa kuwasilishwa kwa wananchi kila baada ya miezi mitatu, na kuagiza taarifa hiyo iandikwe na kuwasilishwa kwake upya na kwa usahihi na ikibainika kuna upotevu wa fedha yoyote,viongozi hao watawajibika kuzirejesha na watachukuliwa hatua.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amewataka watendaji katika wilaya hiyo kuwa makini na suala la mapato kwani ndio chanzo cha maendeleo ya taifa na kuwaagiza kuwasomea wananchi taarifa za mapato na matumizi kwa wakati,kwani ni haki yao kwa vile ndio wachangiaji.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post