Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Man City dhidi ya Burnley utakaochezwa kesho November 26 2016, kocha wa Man City Pep Guardiola ameweka wazi taarifa za wachezaji wake wanaoripotiwa kuwa majeruhi.
Guardiola ameweka wazi kuhusu wachezaji wake Sergio Aguero, Zabaleta na beki wake wa kati na nahodha wao Vincent Kompany, Guardiola ameweka wazi kuwa Kompany ambaye aliumia goti katika mchezo dhidi ya Crystal Palace uliomalizika kwa ushindi wa 2-1, atakuwa nje kwa wiki nne hadi sita.
“Sergio Aguero hajaumia anatatizo dogo tu katika mguu wake na Zabaleta pia tutajua tukifanya mazoezi leo, lakini Vincent Kompany atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne hadi sita, tuna njia nyingi za kuziba pengo lake lakini Toure pia anaweza kucheza beki wa kati”