Shirikisho la kandanda ulimwenguni (FIFA) limetoa orodha ya viwango bora vya soka ,ambapo mpaka sasa kwa upande wa bara la Ulaya Argentina bado ndio taifa bora duniani kwa mujibu wa viwango vya ubora duniani iliyotolewa Ijumaa.
Brazil, chini ya kocha wao mpya, inakuja moto na kuinyemelea kwa kasi.
Kwa upande wa Afrika Senegal ndio vinara na ipo nafasi ya 33 ulimwenguni , huku wakifuatwa na Ivory Coast katika nafasi ya pili ambapo wanafungana na Tunisia kwenye Nafasi hiyo na nafasi ya 36 ni Misri na wapo nafasi ya 34 ulimwenguni.
Nafasi kumi bora Argentina, Brazil, Ujerumani, Chile, Ubelgiji, Colombia, Ufaransa , Ureno, Uruguay, Hispania.
Orodha nyengine ya Fifa ya ubora duniani itatolewa Disemba 22.