Muwakilishi wa Tanzania katika shindano la Miss Afrika 2016, Julitha Kabette, kesho Jumamosi ya November 26 atapanda jukwaani na washiriki wengine 18 kuwania taji la Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.
Mashindano hayo yatafanyika Nigeria katika jimbo la Cross River, mjini Calabar mshindi wa kwanza atapewa zawadi ya dola za Kimarekani 25,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 5o pamoja na gari jipya.
Mshindi wa pili wa shindano la Miss Afrika 2016 atapata zawadi ya dola za Kimarekani 15,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 30 na mshindi wa tatu atapata dola 10,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 20, Julitha Kabette amepata nafasi ya kushiriki mashindano hayo baada ya kuchaguliwa na kampuni ya Millen Magese Group (MMG).