Msikiti wa Haydar Kadı ulioko mjini Manastır kusini magharibi mwa Macedonia ambao ni wa utawala wa zamani wa Ottoman unatarajiwa kufunguliwa tena upya hivi karibuni.
Shughuli za ukarabati wa msikiti huo zilizoanzishwa mwaka 2015 zimekamilika.
Msikiti wa Haydar Kadı ulijengwa wakati wa utawala wa mfalme Kanuni Sultan Süleyman kati ya mwaka 1561-1562 Macedonia na kufungwa kwa miaka 104.