» »Unlabelled » Watumishi 2 Kagera waliokaidi maagizo ya waziri wa maliasili na utalii wasimamishwa kazi.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Waziri wa maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe amemsimisha kazi afisa mkuu wa hifadhi ya mapori ya taifa yaliyoko mkoani Kagera ya Kimisi, Burigi na Biharamulo Jonathan Msiba pamoja na askari wa hifadhi ya mapori hayo Bigirwamungu Kagoma kwa kukaidi maagizo aliyotolewa na waziri huyo yaliyowataka kuwaachia bila masharti Ng’ombe zaidi ya 420 waliowakamatwa katika mapori hayo.

Kauli ya kuwasimamisha kazi watumishi hao imetolewa na naibu waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Lamo Makani ambaye pia aliyejionea makundi ya Ng’ombe yanayomilikiwa na wafugaji 4 yaliyokuwa yamekamatwa na kuhifadhiwa kwenye zizi moja ndani ya pori la Burigi, waziri huyo aliyeongozana na kamati ya bunge inayoshughulikia masuala ya ardhi, maliasili na utalii, akizungumza amesema watumishi hao wamesimamishwa ili wapishe uchunguzi wa kukiuka kanuni za utumishi wa umma ambayo ni pamoja na kukiuka maagizo ya waziri mwenye dhamana.
  
Akijitetea baada ya kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili afisa mkuu wa hifadhi ya mapori ya Taifa ya Kimisi, Burigi na Biharamulo Jonathan Msiba amesema aliwakamata Ng’ombe kwa lengo la kusimamia sheria za nchi, naye mbunge wa jimbo la Biharamulo Osca Mkassa akizungumza amesema suala la kusimamishwa kwa watendaji hao kuwa halina uhusiano na masuala ya siasa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post