» »Unlabelled » Watu 50 wauawa kwenye mapigano Malakal, Sudan Kusini

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


 Uhasama kati ya Dkt Riek Machar na Rais Salva Kiir uliibuka tena Julai mwaka huu

Zaidi ya watu 50 wanaripotiwa kuuawa kufuatia mapigano mapya yaliyozuka nje ya mji wa Malakal nchini Sudan Kusini.

Vikosi vya waasi viliendesha mashambulizi kwenye mji huo wa pili kwa ukubwa siku ya Ijumaa, baada ya kuteka vijiji vilivyo karibu.

Hata hivyo serikali inasema kuwa wanajeshi wake wamewatimua waasi hao hatua iliyosababisha maafa mengi.
Sudan Kusini imekumbwa na misukosuko tangu kujipatia uhuru 2011

Msemaji wa waasi aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa wana matumaini ya kuteka mji wa Malakal na kuongeza kuwa hakuna matumaini ya kuwepo makubaliano kati ya kiongozi wao Riek Machar na rais Salva Kiir pamoja na kati ya kabila la Nuer na lile la Dinka.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post