SERIKALI imetoa vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo wa 2016/2017.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya alisema Dar es Salaam jana kuwa vigezo hivyo vinazingatia Dira ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Sera ya Elimu na Mafunzo (2014) na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Waziri huyo alisema serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, imekuwa ikiwakopesha wanafunzi wenye sifa za kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini kugharamia masomo yao.
Alisema katika utekelezaji wa jukumu hilo, Serikali huandaa sifa na vigezo vya utoaji mikopo kila mwaka ili kuendana na malengo na matarajio yaliyopo katika mipango na mikakati ya kitaifa kama ilivyoainishwa katika mipango mbalimbali. Alisema kwa kuzingatia mipango mikakati na sera hizo, pia Mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka 2016/2017 katika mwaka wa masomo 2016/17 umetolewa.
“Vipaumbele vya kitaifa vinayoendana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na mafunzo ambayo yatazalisha watalaamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele kama vile fani za Sayansi za Tiba na Afya na fani ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati.
Waziri Manyanya alisema vipaumbele vingine ni Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia, Sayansi Asilia na Mabadiliko ya Tabianchi na Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
Alieleza vipaumbele vingine kuwa ni uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji maalum kama vile ulemavu na uyatima na ufaulu wa waombaji katika maeneo ya vipaumbele na umahiri.
“Kwa hivi sasa Bodi imekamilisha uchambuzi wa majina ya waombaji ambao wana sifa zilizoainishwa hapo juu na majina ya wanufaika wapya yatatangazwa. “Aidha, kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo) watakopeshwa kulingana na uwezo wao (means tested) katika vipengele vyote vya mikopo,” alisema.