Dar es Salaam. Wakati anainga Yanga Simon Msuva akifurahia rekodi ya kufikisha mabao 50 tangu aanze kuichezea Yanga, wachezaji wa zamani wamesema kuna tatizo la utunzaji wa rekodi za wachezaji.
Msuva alifikisha mabao 50 katika mchezo baina ya Yanga na Mtibwa ambao timu ilishinda mabao 3-1 na rekodi yake imeibua mjadala kutoka kwa wachezaji wa zamani hususan waliokuwa wakicheza nafasi ya ushambuliaji.
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa, Abeid Mziba aliliambia gazeti kuwa miaka ya nyuma Tanzania ilikuwa na wafungaji wengi, lakini rekodi zao hazipo kutokana na kutokuhifadhiwa.
“Sikumbuki mabao niliyofunga, ni mengi kuzidi hata 50 ya Msuva.
Nimecheza Yanga kwa miaka 11 na nilikuwa. Sidhani kama kuna rekodi za miaka ya nyuma,” alisema Mziba aliyekuwa mtaalamu wa kufunga mabao kwa kutumia kichwa.
Straika wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel alilitupia lawama Shirikisho la Soka Tanzania, TFF kwa kushindwa kutunza takwimu za wachezaji na idadi ya magoli waliyofunga. “Nimecheza Simba katika vipindi totauti kwa miaka 11. Nilifunga zaidi ya magoli 60 lakini hakukuwa na mfumo wa kutunza takwimu za wachezaji. Inatakiwa wachezaji wa sasa wajitambue kwa takwimu na zitawasaidia kupiga hatua,” alisema Gabriel ambaye enzi zake akiwa Simba alikuwa muuaji wa mara kwa mara wa Yanga. Naye Edibily
Lunyamila aliyeichezea Yanga kwa miaka 11 na kufunga zaidi ya mabao 50 alisema: “Wachezaji wa zamani wamefunga mabao mengi tu lakini nani anatunza takwimu zao? Hata Msuva yawezekana takwimu hizi kazihaangaikia mwenyewe.”
Athuman Machuppa aliyeitumikia Simba kwa muda mrefu alisema ni muhimu wachezaji wa sasa kutunza kumbukumbu zao zitakazowasaidia kupata fursa ya kucheza soka sehemu mbalimbali duniani. Machuppa kwa sasa anachezea klabu ya Kilimanjaro ya Sweden. Wakati Saady Kawemba akiwa mkurugenzi wa mashindano wa TFF kitengo hicho kilianza kufanya kazi ya kutunza rekodi za wachezaji.