» »Unlabelled » Shiwata Yandaa Mashindano

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)umeandaa mashindano ya Sanaa na Michezo litakalofanyika kuanzia Novemba 12,2016 katika viwanja
mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema jana kuwa michezo
itakayoshindaniwa ni soka,mpira wa kikapu,ngoma za asili, muziki wa
dansi, sarakasi, Karate na kaswida.

Alisema mashindano hayo yatafanyika kuwapata washindi ambao kwa pamoja watakwenda kukabidhiwa zawadi zao kwenye kijiji cha wasanii
Mwanzega,Mkuranga.

Mwenyekiti Taalib aliwataja wajumbe wa Kamati ya tamasha hilo kuwa ni
Deo Kway, na mchezaji wa zamani wa Simba, Kureshi Ufunguo na mchezaji
wa zamani wa Yanga, Salvatory Edward watakaosimamia mashindano ya
soka.

Wengine ni Selemani Pembe, Athumani Bakari maarufu kama Mbegeja katika mchezo wa sarakasi,Abdul Salvador kamati ya muziki wa dansi na Kocha wa timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu, Manase Zablon katika mchezo wa mpira wa kikapu.

Wajumbe wengine ni Ismail Kambangwa, Kashindye Fundikira na Mariam
Ismail maarufu kama mama Mipango watakaosimamia ngoma za asili.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post