» »Unlabelled » Shein: Tupo tayari kukosa misaada yenye masharti

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Dar es Salaam. Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya ZanzibarDk Ali Mohamed Shein amesema Serikali zote mbili ikiwamo ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania zipo tayari kustahili kukosa misaada inayotolewa kwa masharti yenye lengo la kuharibu maendeleo ya nchi au usalama.

Dk Shein ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar ameyasema hayo leo mkoani Simiyu  kwenye sherehe za maadhimisho ya kilele  chaMbio za Mwengewa Uhuru, ambazo huambatana na Maadhimisho yaSiku yaKumbukumbu ya Muasisi wa Taifa  na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki miaka 17 iliyopita.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyorushwa moja kwa moja kwenye vituo kadhaa vya luninga Dk Shein amesema Serikali hizo zimejipanga kutumia vizuri mapato yake inayokusany, ili kupunguza utegemezi wa misaada kutoka kwa wahisani.

“Wapo baadhi ya wahisani wa maendeleo hutoa misaada kwa masharti yasiyotekelezeka , hatupo tayari kupokea misaada ya aina hiyo tutashahilimi kuliko kudhalilishwa tutajitegemea, tutakaribishwa misaada ya wahisani ambao watatusaidia bila masharti hayo,” amesema Dk Shein.      

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post