» »Unlabelled » Kaokoa maisha ya mchezaji mwenzake, ila FIFA wanamchunguza staili yake ya ushangiliaji

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 Beki wa klabu ya Paris Saint Gemain ya Ufaransa anayeichezea timu ya taifa ya Ivory Coast Serge Aurier weekend iliyopita alipongezwa na watu wengi wa soka hususani kwa kitendo chake cha kijasiri cha kuokoa maisha cha mchezaji wa timu ya taifa ya Mali Moussa Doumbia.

Serge alipongezwa na watu wengi baada ya kumsaidia Doumbia asimeze ulimi wake kufuatia kupoteza fahamu uwanjani, kitendo ambacho kingeweza kumfanya Doumbia apoteze maisha, licha ya kitendo hicho cha kijasiri FIFA wametoa statement ya kufanya uchunguzi kwa nini Serge alishangilia staili kama ya kuchinja baada ya kufunga goli.

 Beki huyo ambaye amewahi kuingia katika headlines ikiwemo kudaiwa kumtukana kwa lugha ya ishara kocha wa PSG Laurent Blanc, alifunga goli katika ushindi wa goli 3-1 kati ya Ivory Coast dhidi ya Mali na kuweka mkono kwenye shingo na kuuchezeshachezesha kama kisu wakati akishangilia goli.

Hapa wakati akishangilia goli lake kwa staili iliyofanya FIFA watangaze kuanza kufanya uchunguzi

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post