» »Unlabelled » Polisi Kutoa Taarifa Ya Kifo Cha Mwanamasumbwi Thomas Mashali Siku Ya Jumatano

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa wanaendelea na upelelezi kwa kufuatia kuuawa kwa mwanamasumbwi Thomas Mashali na watatoa taarifa ya kifo hicho siku ya Jumatano.

Akizungumza na waandshi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro amesema taarifa zilizopo kwa kufuatia kifo cha bondia huyo ni za kufikirika na zinasemwa tu, hivyo Jumatano nitatoa taarifa hiyo.

Kamishina Sirro amesema kuwa bondia huyo ni mtu mkubwa na hakuna mtu aliethibitisha kuwa ni mny'ang'anyi, hivyo mpaka sasa ni maneno ya mtaani tu.

“Mimi ndio napata taarifa juu ya kifo cha bondia huyo. Ngoja nisubiri taarifa niweze kutoa siku ya Jumatano, ambapo nitakuwa na majibu sahihi. Kwa leo niache tu”amesema Kamishna Sirro.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post