» »Unlabelled » Mtoto kukojoa kitandani

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Wiki hii kwenye safu yetu nitakuandikia tiba ya mtoto kukojoa kitandani, kitu kinachosumbua wazazi wengi.

Dawa tunazo majumbani, lakini hatujui jinsi ya kuzitumia. Leo nitakuonesha tiba tofauti zitakazosaidia kumaliza tatizo.

Mafuta ya mzaituni
Kama mwanao ana tatizo hilo, chukua mafuta haya yapashe kidogo kisha mlaze mwanao, umpake yakiwa na vuguvugu chini ya kitovu kisha umfanyie masaji.
Mdalasini

Hakikisha mwanao anatafuna mdalasini kwa siku hata mara moja, kama hawezi kuutafuna chukua unga wake, changanya na sukari kisha weka kwenye mkate wenye mafuta mpe mwanao.
Ni tiba nzuri ambayo inasaidia haraka tatizo hilo.

Matunda damu
Mpe mwanao glasi ya juisi ya matunda damu saa moja kabla ya kulala, tumia tiba hii kila siku angalau kwa wiki kadhaa.

Kama ataendelea, mpe nusu kikombe kwa siku mara tatu, iwe kama dozi ya vidonge.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post