» »Unlabelled » ‘Msuva airushia Simba SC jiwe’

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Dar es Salaam. Winga wa Yanga, Simon Msuva amesema kadri ligi inavyoendelea wanarejesha ubora wao na kuwapa onyo waliokalia usukani kuwa wanakuja kwa kasi kuchukua nafasi yao.

Msuva aliliambia gazeti hili kuwa hawakuanza ligi vizuri kutokana na uchovu, lakini kadri muda unavyoenda wanazidi kuimarika na kurudi katika ubora wao.

Mchezaji huyo ambaye amefikisha mabao 50 tangu aanze kuichezea timu hiyo mwaka 2012, alisema kila mara wameendelea kupambana ili kuhakikisha wanatetea ubingwa wao msimu huu na anaamini waliopo juu ni kama wamewashikia nafasi.

“Tumeanza ligi kichovu kwa sababu tumechoka sana na hatukupata muda wa kupumzika tangu ligi ya msimu uliopita imalizike, jambo hilo limesababisha tusicheze soka letu lililozoeleka.

“Hata hivyo, ligi inavyoendelea tunazidi kuimarika na kurudi katika ubora wetu na sasa tunaanza kucheza ule mpira wetu na naamini tutaendelea hivi hata katika michezo ijayo,” alisema Msuva.

Aliongeza: “Najua wapinzani wetu wanaongoza ligi hata sisi tunakuja huko huko juu, muda si mrefu tutarejea kwenye nafasi yetu tunayostahili, hivyo waache waendelea kufurahia lakini ubingwa msimu huu wa Yanga.

Yanga iko nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 14 baada ya kucheza michezo saba, imeshinda minne, imetoa sare miwili na kupoteza mmoja.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post