» »Unlabelled » Manji aita viongozi wa matawi Jangwani

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Dar es Salaam. Siku saba kabla ya kufanyika mkutano wa kuamua hatima ya klabu ya Yanga kukodishwa kwa mwenyekiti, Yusuf Manji, kiongozi huyo ameitisha mkutano wa dharura na wenyeviti wa matawi kujadili ajenda za mkutano huo.

Mkutano huo ulifanyika jana Makao Makuu ya klabu katika mitaa ya Twiga na Jangwani.

Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit alisema mkutano mkuu wa Oktoba 23 ndiyo utaamua hatima ya kukodishwa kwa klabu hiyo au la.

“Ajenda ya kukodisha klabu itapitishwa na mkutano mkuu ujao, akidi ikitimia kwa mujibu wa katiba yetu ndipo shughuli hiyo itafanyika,” alisema Baraka na kufafanua kuwa: “Yanga ‘inadili’ na wanachama wanaolipia kadi zao, wapo wenye kadi, lakini hawazilipii hao siwezi kuwazungumzia kwa sababu si wanachama hai.”

Wakizungumza na Mwananchi jana makao makuu ya klabu hiyo, baadhi ya wajumbe walisema Manji alitumia kikao hicho kupata maoni mbalimbali ya viongozi wa matawi na kujadili agenda za mkutano ujao.

Huo ni mkutano wa kwanza wa Manji na viongozi wa matawi baada ya wiki mbili za hoja mbalimbali kutolewa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu uhalali wa mwenyekiti huo kukodishwa klabu hiyo kwa miaka 10.

Mkutano huo wa jana, ulidumu kwa saa moja nusu hadi kumalizika.

Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, Hassan Msigiti ambaye ni mwenyekiti wa Yanga tawi la Ubungo alisema mkutano huo ulijikita kujadili ajenda za mkutano ujao ambazo zitatangazwa baada ya mwenyekiti kukutana na kamati ya utendaji.

Alipohojiwa ikiwa mkutano huo utatumika kumkabidhi Manji timu na nembo Msigiti alisema: “Wanachama tulishampa Manji timu hao, hao TFF na wengine wanaoingea sana, lakini wajue Yanga tulishafanya uamuzi.”

Hata hivyo, gazeti hili lilishuhudia baadhi ya wajumbe wakisema hawakubaliani na utaratibu uliotumika katika kikao hicho na watapinga uamuzi utakayofanywa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post