Msanii MR. Blue aliyeshika Mic akiwa pamoja na Abby Skills waliposhiriki FNL
Msanii wa Bongo Fleva nchini Mr. Blue ameweka bayana kwamba pamoj na kukubalika na mashabiki wengi na na kuwa kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu hajawahi kupata tuzo hata moja ya kutambua mchango wake kwenye muziki.
“Mimi sijawahi kupata tuzo yoyote siyo ya kitaifa wala ya kimataifa ila ninachoamini mimi ni kwamba mimi ni ‘expensive’ na ndiyo maana natoa ngoma mara moja kwa mwaka na inadumu kwa muda mrefu” Amesema Mr. Blue
Aidha Mr. Blue ameongeza kuwa tuzo ambazo zimeanzishwa na EATV zitasaidia sana wasanii wengi kuweza kutambulika zaidi na anaamini pengine anaweza kupata tuzo hiyo na ikawa tuzo yake ya mara ya kwanza.
