Mwanza. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba amesema anao ushahidi wa kujitosheleza kuhusu taarifa aliyotoa kwa waandishi wa habari ofisini kwake Septemba 27, mwaka huu.
Siku hiyo, inadaiwa kuwa Kibamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa walimu hao wakuu wa shule za msingi na sekondari wameidanganya Serikali na kuisababishia hasara ya mamilioni ya shilingi.
Walimu hao kupitia Chama chao cha Walimu Tanzania (CWT), juzi kilipiga hodi Idara ya Utumishi wa Walimu (TSD) wilayani Nyamagana mkoani Mwanza kwenda kumshtaki mkurugenzi huyo kwa madai amewadhalilisha.
Kibamba alisema: “Kimsingi mimi ndiye ninatakiwa kulalamikia walimu hao mbele ya TSD. Nasubiri kuitwa ili niwasilishe ushahidi nilionao dhidi yao.”
Katibu wa TSD Wilaya ya Nyamagana, Peninah Alphonce alisema walimu 37 wa shule za msingi na 62 wa sekondari wanadai kudhalilishwa kwa tuhuma za kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh100 milioni baada ya kusajili wanafunzi hewa zaidi ya 8,000.
Katibu wa CWT Nyamagana, Asha Juma alisema msimamo wao upo palepale.
“Hata kama TSD watasuasua kushughulikia malalamiko yetu, CWT tunawasiliana na mawakili kwa ajili ya kumfikisha mkurugenzi mahakamani kwa vile ameshindwa kukanusha ndani ya muda wa siku tatu tulizompatia,” alisema.