» »Unlabelled » Mkono awaponda watayarishaji wa filamu nchini

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Mchekeshaji na muigizaji maarufu nchini Mkono Mkonowe amefunguka na kusema kuwa tasnia ya filamu nchini inashuka sana kwa sababu watayarishaji wengi wa filamu nchini kwa sasa hawatumii ubunifu mkubwa katika kutayarisha kazi hizo.

eNewz ilipiga story na mchekeshaji huyo na alisema kuwa tasnia ya filamu nchini inazidi kudidimia kwa sababu watayarishaji wenyewe hawatumii ubunifu na pia wengi wao wanaendekeza unywaji wa pombe bila kujali kile wanachotakiwa kukifanya

"Kwa sasa tasnia ya filamu nchini imeshuka sana watayarishaji wengi wamekuwa siyo wabunifu katika kazi zao wengi wanakwambia mimi ukininunulia tu pombe nakumalizia kazi yote tofauti na watayarishaji wa zamani walikuwa wanaangalia ubora wa kazi ndiyo mana filamu za zamani nyingi zilikuwa na viwango tofauti na sasa." alisema Mkono

Pia aliongeza kwa kusema kuwa yuko mbioni kuachia movie yake ambayo amecheza kwa kihindi hivyo mashabikli wake wakae tayari kwa movie hiyo itakayotoka hivi karibuni.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post