» »Unlabelled » Mavugo asema mambo ni magumu

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Mshambuliaji Laudit Mavugo raia wa Burundi, bado hajafikia kile kiwango ambacho Watanzania wengi wapenda soka hasa wale wa timu ya Simba walikuwa wakikitarajia.Tokeo la picha la mavugo simba

Hali hiyo imezua maswali mengi na wakati mwingine inamuonyesha yeye kupaniki akitaka kuwaonyesha anaweza.

Lakini baadaye amekubali, kwamba anahitaji muda ili ikifika siku, ataonyesha alichonacho.
Mavugo ambaye alisajiliwa Simba akitokea Vital’O ya kwao Burundi, mara ya mwisho kufunga bao ilikuwa ni Oktoba 23 dhidi ya Toto kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar lakini kabla ya hapo alikuwa amecheza mechi sita mfululizo bila kufunga bao lolote.

Juzi Jumamosi kwenye mchezo dhidi ya Mwadui mjini hapa alishindwa tena kucheka na nyavu. Alipata nafasi kibao lakini alizipoteza kabla ya kocha Joseph Omog kumtoa katika dakika ya 42 kipindi cha kwanza.

Baada ya mchezo huo, Mavugo ambaye alianza ligi kwa mbwembwe na kuonekana atakuwa supastaa wa Simba, alisema: “Hakika naomba mashabiki wa Simba wanipe muda kwani bado sijazoea baadhi ya viwanja vya hapa Tanzania, kwani kuna viwanja vizuri lakini pia vingine ni vibovu. 

“Kule kwetu Burundi hakuna viwanja vibovu kama huku Tanzania, ndiyo maana kule nilikuwa nafunga mabao mengi lakini huku napata tabu sana jinsi ya kufunga lakini nina imani kuwa nitayazoea mazingira na nitafanya vema.”

Juzi, Mavugo ambaye msimu huu tayari ana mabao manne, alikosa mabao matatu ya wazi na kulazimika kutolewa nje mapema kabisa na nafasi yake ikachukuliwa na Ame Ally aliyeiimarisha safu ya ushambuliaji ya Simba huku akitoa pasi ya bao la tatu la klabu hiyo lililofungwa na Mohammed Ibrahim.

Pamoja na papara, Mavugo amekuwa akionyesha ni mchezaji anayeweza kufanya vizuri zaidi ya alipofikia lakini papara ya kutaka kuwaonyesha wanaofikiri hawawezi wamekosea, inachangia kwa kiasi kikubwa yeye kushindwa kufanya vema kama anavyotaka.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post