» »Unlabelled » Kesi ya kuchoma kituo cha polisi yapigwa tena kalenda

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

KESI ya kuchoma moto Kituo cha Polisi Bunju ‘A’ imeahirishwa hadi Novemba 10 na 11, mwaka huu, itakapoendelea kusikilizwa ushahidi wa utetezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.


Jana mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, ilipanga kusikiliza ushahidi wa utetezi lakini wakili wa serikali anayeendesha kesi hiyo amepata udhuru wa kikazi.

Hakimu Simba alisema kesi hiyo ni miongoni mwa zinazotakiwa kumalizika kabla ya Desemba, mwaka huu, na kwamba upande wa Jamhuri ufanye juhudi kuhakikisha tarehe zilizopangwa kesi hiyo inasikilizwa.

Kabla ya kuahirishwa kesi hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi, alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa lakini wakili anayeendesha kesi hiyo amepata udhuru wa kikazi.

Source: Nipashe
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post