» »Unlabelled » Jeshi la Nigeria Lawaachilia Watoto 876

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

 NIGERIA: Umoja wa Mataifa umefanikisha kuachiliwa kwa watoto 876 wanaozuiliwa na wanajeshi wa Nigeria na vikosi vya usalama baada ya kuteka ardhi iliyokuwa ikikaliwa na Boko Haram.

Watoto hao wamekuwa wakizuiliwa katika kambi za kijeshi kwenye mji wa Maiduguri ulio Kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wanajeshi huwazuilia raia ambao wamekuwa wakiishi maeneo ambayo yamekuwa yakikaliwa na wanamgambo wa kiislamu, kwa kuwashukuwa kwa wana uhusiano na shughuli za wanamgambo hao.

Hata hivyo makundi ya kibinadamu yanalalamika kuwa hakuna sheria ya kuwafungulia mashtaka watu hao.
Baadhi yao hupelekwa kwa vituo vya kurekebisha tabia ambavyo makundi ya kibinadamu yanasema kuwa vinafanana na magereza.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post