» »Unlabelled » Guardiola arusha kijembe cha chini chini kwa Man United kwa matumizi ya mipira mirefu

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Pep Guardiola ameendelea kuwachimba Manchester United chini chini kwa matumizi yao makubwa ya mipira ya mirefu na kudadavua anachopenda hasa kifanyike kwenye timu yake.

Guardiola leo atakuwa na kibarua kigumu mbele ya West Brom kwenye dimba la Hawthorns, mchezo ambao utakuwa mgumu kwake kufuatia kucheza michezo sita mfululizo bila ushindi, rekodi ambayo ni mbaya zaidi kuwahi kutokea katika maisha yake ya ukocha.

Man City walifungwa bao 1-0 dhidi ya mahasimu wao Man United katika Uwanja wa Old Trafford katikati ya wiki hii kwenye mchezo wa Kombe la EFL.

“Goli tulilofungwa katika mchezo dhidi ya United lilitokana na mpira mrefu, tukashindwa kuudhibiti na hatimaye tukafungwa.

“Wakati mwingine unaruhusu goli kwasababu umeshindwa kuzuia mipango ya goli kama ilivyotokea kwetu na wakati mwingine unaweza kutumia pasi ndefu na ukaruhusu goli vile vile.

Guardiola alienda mbali zaidi kwa kusema: “Kwa aina ya washambuliaji tulio nao kama Kelechi, Kun Aguero, si vyema kwangu kutumia pasi ndefu, labda kwa siku zijazo nikinunua straika mwenye urefu wa sentimeta 220 nitaweza kutumia mfumo huo.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post