» »Unlabelled » "Bi Clinton afanyiwe majaribio ya Dawa" Trump asema

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Mgombea kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amemshutumu mpinzani wake Bi Hillary Clinton kwa kutumia aina fulani ya dawa, wakati wa mjadala wao uliopita wa moja kwa moja wa runinga.

Anasema kuwa alikuwa na haiba mwanzo mwanzo wa mjadala huo.

Sasa anapendekeza kuwa wafanyiwe majaribio ya matumizi ya dawa, kabla ya kufanyika kwa mjadala wao wa mwisho hapo siku ya Jumatano ya wiki hii.

Katika mkutano wake wa hivi punde uliofanyika New Hampshire, Bwana Trump kwa mara nyingine, amedai kuwa kuna njama za kumuibia kura.

Timu ya kampeini ya Bi Clinton, imesema kwamba wapigaji kura, sasa wameona bayana kile anachokiita juhudi za aibu za Bwana Trump za kutaka kuhujumu shughuli za upigaji kura.

Trump, anazidi kudidimia katika majimbo mengi, huku akikabiliwa na madai ya udhalalalishaji wanawake kingono.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post