» »Unlabelled » Azuiwa kufanya mtihani kwa kufunga hijabu Canada

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Mwanafunzi mmoja wa Kiislamu ameripotiwa kufukuzwa shuleni na kuzuiwa kufanya mtihani na mwalimu mmoja baada ya kukataa kuvua hijabu shuleni nchini Canada.

Azuiwa kufanya mtihani kwa kufunga hijabu Canada


Tukio hilo lilizuwa utata baada ya kutokea kwenye shule ya upili ya College de Maisonneuve iliyoko mjini Montreal.
Msemaji wa shule hiyo Line Legare alitoa maelezo na kusema, ‘‘Mwalimu wetu wa somo la biyolojia aliwahi kutangaza mwanzoni mwa mwaka kwamba hatoruhusu wanafunzi wake kuingia kwenye mtihani wakiwa na kofia, mtandio au hijabu vichwani. Mwalimu huyo alimfukuza mwanafunzi kutokana na ukiukaji wa sheria iliyowekwa kwa hofu ya uwezekano wa kulaghai kwenye mtihani.’’
Maelezo zaidi yamearifu kwamba mwanafunzi huyo alifukuzwa baada ya kukataa kuvua hijabu kutokana na sheria za imani ya dini yake ya Kiislamu.
Legare aliongezea kuwa tukio hilo limemkera mwalimu na hivyo basi, wanaendelea kujadili ili mwanafunzi huyo aweze kufanya mtihani katika tarehe nyingine.
Legare pia alisema kwamba mwanafunzi huyo bado hajawasilisha rasmi mashtaka dhidi ya mwalimu na kwasasa utawala wa shule unafanya mazungumzo ili kuhakikisha tukio kama hilo halirudiwi tena.
Kwa upande mwingine waziri mkuu wa mkoa wa Quebec Philippe Couillard naye alitoa maelezo na kubainisha kuridhishwa kwa utatuzi wa mzozo huo huku akiahidi kuwasilisha muswada bungeni kuhusu tukio hilo.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post